Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala ya rambi-rambi kwa jamaa, ndugu na marafiki wa kabaila Shameem Ahmed ambaye amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu Shameem Ahmed ni mama mkwe wa Waziri wa Elimu balozi Amina Mohamed.
Kwenye risala yake, Rais Kenyatta alisema Mama Shameem Ahmed alikuwa mwanamke shupavu na raia aliyeheshimika ambaye alitumikia taifa hili kwa ustadi.
Rais Kenyatta alisema Mama Shameem Ahmed alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kufanya kazi katika huduma ya umma ambaye aliamini na kutetea elimu kwa wasichana.
“Bila shaka, Mama Shameem Ahmed alikuwa mmoja wa wanawake mashuhuri wakati wa enzi yake. Alikuwa mama mkuu aliyejitolea kutumikia familia yake na taifa,” kasema Rais Kenyatta.
Huku akiongeza kusema: “Alikuwa miongoni mwa wanawake wa kwanza kujiunga na huduma ya umma, hasa katika utoaji elimu. Aliamini kuwa wasichana hawapaswi kuachwa nyuma na kwamba wasichana wana uwezo wa kugeuza ulimwengu.”
By PPS